Mlima rungwe
ni mlima ulipopo katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Inaaminika kwamba mlima huu ulitokana na volcano iliyozimika kusini kusini magharibi mwa Tanzania, Ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita. Ukiwa na kimo cha 2960 m ni mlima mkubwa kusini mwa Tanzania na ni wa tatu kwa ukubwa Tanzania
Mlima Rungwe
Mlima Rungwe ukionekana kwa mbali kama picha ilivyochukuliwa kutoka The green city Profile
Mlima unasimama juu ya ncha ya kaskazini ya Ziwa nyasa. Upande wa kusini-mashariki wa mlima hupokea usimbishaji wa 3,000 mm kwa mwaka ambao ni juu kabisa katika Tanzania.
Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutba na kilimo. Rungwe ni eneo la Wanyakyusa.Jina la mlima limekuwa pia jina la wilaya ya Rungwe
Katika mlima rungwe kuna viumbe hai mbali mbali kama ndege na wanyama. Moja ya
wanyama wanaopatikana katika mlima rungwe ni nyani ambapo kuna aina moja ya
nyani wanaopatikana mlimani hapo tu ambao wanajulikana kama kipunji.
Nyani aina ya kipunji wanaopatikana mlima Rungwe tu
Ukiwa juu
yam lima rungwe unaweza kuliona ziwa nyasa vizuri pamoja na mbuga ya wanyama
kitulo. Upande wa kusini mwa mlima utaona ziwa nyasa na upande wa mashariki
utaona bonde la kitulo.
Ziwa Nyasa

Kitulo National Park



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni