Habari Za Hivi Punde

Alhamisi, 27 Februari 2014

ZIWA MASOKO


Ziwa masoko ni ziwa lililopo katika halimashauri ya wilaya ya busokelo mkoani Mbeya nchini Tanzania.Ziwa masoko linaonekana kwa urahisi ukitokea Tukuyu na ni kilometa 15 ukiwa njiani kuelekea Ipinda na liko jirani kabisa na barabara.



Ziwa masoko ni zuri kwa utalii na lina fukwe nzuri kwa ajili ya kupumzikia pamoja na kuogelea na pia lina maji safi na salama na pia ziwa masoko limezungukwa na miti iliyostawi na kumea vizuri inayoongeza uzuri wa ziwa hili


Kwa mujibu wa historia inasemekana kwamba wajerumani walijenga ngome yao hapo katika vita ya pili ya dunia(2WW) na kabla hawajafukuzwa na waingereza wakaamua kutumbukiza vitu vyao vya thamani ziwadi . 

Inawezekana kukawa na ukweli ndani yake kwa sababu mara nyingine sarafu za zamani za kijerumani huwa zinaonekana ufukweni baada ya kuibuliwa na maji kutoka ziwani. 


Maoni 2 :

  1. hiki kisiwa kinasemekana kiliwai tokea na maajabu ya kuwepo nyoka mwenye vichwa kama sikosei 12 na inasemekana aliuawa na mzungu na alipo toka nje ya mtumbwi yule mzungu na akafariki na makabuli ya mzungu na huyo nyoka yako hapo je ni yakweli?

    JibuFuta

Designed By