Ziwa
masoko ni ziwa lililopo katika halimashauri ya wilaya ya busokelo mkoani Mbeya
nchini Tanzania.Ziwa masoko linaonekana kwa urahisi ukitokea Tukuyu na ni
kilometa 15 ukiwa njiani kuelekea Ipinda na liko jirani kabisa na barabara.
Ziwa
masoko ni zuri kwa utalii na lina fukwe nzuri kwa ajili ya kupumzikia pamoja na
kuogelea na pia lina maji safi na salama na pia ziwa masoko limezungukwa na
miti iliyostawi na kumea vizuri inayoongeza uzuri wa ziwa hili
Kwa
mujibu wa historia inasemekana kwamba wajerumani walijenga ngome yao hapo
katika vita ya pili ya dunia(2WW) na kabla hawajafukuzwa na waingereza wakaamua
kutumbukiza vitu vyao vya thamani ziwadi .
Inawezekana
kukawa na ukweli ndani yake kwa sababu mara nyingine sarafu za zamani za
kijerumani huwa zinaonekana ufukweni baada ya kuibuliwa na maji kutoka ziwani.

hiki kisiwa kinasemekana kiliwai tokea na maajabu ya kuwepo nyoka mwenye vichwa kama sikosei 12 na inasemekana aliuawa na mzungu na alipo toka nje ya mtumbwi yule mzungu na akafariki na makabuli ya mzungu na huyo nyoka yako hapo je ni yakweli?
JibuFutaNikweli Ndugu Mwakye
Futa