Moja ya madhumuni ya kutengenezwa kwa blog hii ni kuelezea vivutio vilivyopo ndani ya mkoa wa Mbeya hasa katika wilaya ya Rungwe pamoja na Busokelo, ambapo wilaya ya Busokelo imetoka ndani ya wilaya ya Rungwe. Hii inamaanisha kwamba Busokelo imezaliwa kutoka ndani ya wilaya ya Rungwe ambapo wilaya ya Rungwe imegawanywa mara mbili.
Pia blog yetu itakuletea habari mbali mbali kutoka ndani ya mkoa wa mbeya ikiwemo habari za kijamii, michezo , burudani na shughuli mbali mbali zinazofanyika ndani ya mkoa wetu. Vilevile utapata habari kutoka nje ya mkoa wa mbeya ambapo utapata habari za kitaifa na kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni